Afisa Mkuu wa Marekani amesema nchi hiyo haikutoa taarifa yoyote rasmi kwa utawala wa Syria juu ya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu mapema leo. Msemaji wa Wizara ya mambo ya nchi za nje Bibi Jen Psaki alisema pia kwamba hawakushirikiana kwa njia yoyote na serikali ya Syria katika utekelezaji wa mashambulizi hayo.
Hata hivyo Psaki alisema utawala wa Syria uliarifiwa moja kwa moja kupitia Balozi wa Marekani katika Umoja wa mataifa Samantha Power, aliyempa taarifa Mwakilishi wa kudumu wa Syria katika Umoja huo. Awali Syria ilisema inaunga mkono hatua yoyote ya kijeshi dhidi ya wapiganaji wa Dola la Kiislamu.
0 maoni:
Post a Comment