Obama asema nchi yake haiko peke yake katika vita dhidi ya IS
Rais wa Marekani Barrack Obama amesema muungano wa nchi za
kiarabu zilizoshiriki katika shambulizi la kwanza la Marekani katika
mapambano dhidi ya wanamgambo walio na itikadi kali wa Dola la
Kiislamu IS nchini Syria, umeonyesha kuwa Marekani haiko peke
yake katika mapambano kwa wanamgambo hao. Obama pia
ameonya kuwa operesheni dhidi ya kundi hilo huenda ikachukua
muda, lakini atafanya kila liwezekanalo kuwashinda wanamgambo
hao. Mashambulizi hayo ya angani yanayotekelezwa na Marekani na
baadhi ya mataifa ya kiarabu yalianza siku ya jumatatu usiku
yakilenga makao makuu ya wanamgambo wa IS Mashariki mwa
Syria.
0 maoni:
Post a Comment