Na Daniel Mjema na Sharon Sauwa, Mwananchi
Dodoma.
Ofisi
ya Bunge la Katiba itamtuma ofisa wake kwenda Makka, Saudi Arabia
kusimamia upigaji kura kupitisha Katiba inayopendekezwa kwa wajumbe wa
Bunge hilo wanaokwenda Hijja.
Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad
alipotakiwa kueleza idadi kamili ya wajumbe wa Bunge hilo wanaotarajiwa
kuwa nje ya nchi na jinsi watakavyopiga kura.
Juzi, Bunge hilo lilizifanyia marekebisho kanuni zake ili kuwaruhusu
wajumbe watakaokuwa nje ya Ukumbi wa Bunge wakiwamo wanaokwenda Hijja
kuipigia kura Katiba inayopendekezwa, iliyokabidhiwa kwa Kamati ya
Uongozi jana.
Chini ya marekebisho hayo, mjumbe aliye nje ya Bunge, ataruhusiwa kupiga
kura ya wazi au ya siri kwa njia ya fax au mtandao kama
itakavyoelekezwa na katibu kwa kushauriana na mwenyekiti.
Hamad alisema hadi kufikia jana mchana walikuwa wamewatambua wajumbe
wanane ambao watakwenda Hijja huko Uarabuni lakini orodha ya watakaokuwa
nchi nyingine bado haijajulikana.
Hamadi alisema ofisa wake huyo atasimamia kura za wajumbe wanaokwenda
Hijja katika upigaji kura unaotarajiwa kuanza Septemba 29 hadi Oktoba 2
mwaka huu.
Wazanzibari 500,000 kupata vitambulisho
Na Rahma Suleiman
Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) imeanza kutoa vitambulisho vya taifa
kwa wananchi wa Zanzibar ambapo zaidi ya vitambulisho 500,000
vinatarajiwa kutolewa.
Mkurugenzi wa Nida Zanzibar, Vuai Mussa Suleiman, alisema katika zoezi hilo wamejipanga vizuri ili kudhibiti maafa yasitokee kama yaliotokea wakati wa uandikishwaji wa zoezi hilo lililosababisha kifo na majeruhi.
Alisema kwa hatua za awali ugawaji huo umeanzia Mkoa wa Kaskazini Unguja na kuwataka wananchi wanapokwenda kuchukuwa vitambulisho vyao katika vituo walivyopangiwa wachukue stakabadhi au vielelezo walivyopewa wakati wa uandikishwaji.
Alisema kama stakabadhi zao zimepotea, wanatakiwa kuchukua vitambulisho vingine ambavyo walivitumia wakati wa kujiandikisha.

0 maoni:
Post a Comment