Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Lwandai kata ya Mlola ambapo aliwasisitiza wananchi hao kushiriki kazi
za maendeleo na kujiunga kwa wingi kwenye mfuko wa Afya ya jamii.
Umati wa wakazi wa kata ya Mlola wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia wananchi hao.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Lwandai, kata ya Mlola ambapo aliwaambia wawe makini na matapeli wa
ardhi wanaokuja kwa jina la Uwekezaji kwani wamekuwa chanzo kikubwa cha
migogoro ya ardhi nchini.
Wazee
Maarufu wa kijiji cha Lwandai wakifuatilia kwa makini mkutano wa Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anafanya ziara za kujenga
na kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi,Pia katika mikutano yake ya sasa
Katibu Mkuu amekuwa akitoa nafasi kwa wananchi kuhoji maswali ,kutoa
maoni au ushauri kuhusu maendeleo yao katika maeneo yao.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Lwandai kata ya Mlola wilaya Lushoto.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahamn Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na
Uenezi Nape Nnauye kwa pamoja wakiwapungia mkono mamia ya watu
waliofurika kwenye uwanja wa mikutano wa kijiji cha Lwandai kata ya
Mlola wilayani Lushoto.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Lwandai
ambapo aliwaambia wawe makini na maneno ya wanasiaa ambao wanahusisha
hoja ya katiba mpya na uchaguzi wa mwaka 2015, alisema kuwa kuna watu
wana sahau kuwa hiyo siyo ajenda ya wananchi na si makubaliano ya vyama
vya siasa .
Wananchi wa Mlola wakimsikiliza Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Kila kona ya uwanja ilijaza watu.
Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Hemed Mwanga akitoa
ufafanuzi juu ya mambo mbali mbali yanahusu maendeleo ya wilaya hiyo
wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
uliofanyika kwenye uwanja wa mikutano wa kijiji cha Lwandai kata ya
Mlola ,Lushoto mkoani Tanga.
Nyuso za matumaini za wakazi wa Mlola.
Deogratius
Kisandu akiwasalimia wananchi wa Lwandai kata ya Mlola wilani Lushoto
baada ya kujiunga rasmi na Chama Cha Mapinduzi kwenye mkutano wa hadhara
ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana .Deogratius
alishawahi kuwa na nyanzifa zifuatazo kwenye chama cha NCCR
Mageuzi,Katibu Mwenezi Taifa kitengo cha Vijana (2013) na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu Taifa ya NCCR-Mageuzi (2014)
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (katikati) akiondoka eneo la
mkutano huku akiongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye
(kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Mhe. Majid Hemed Mwanga.
Vitalu vya miti kwenye mradi wa upandaji miti Kwesimu.
Katibu
Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka mbole
kwenye vitalu vya mradi wa upandaji miti Kwesimu muda mchache kabla ya
kwenda kwenye mkutano wa hadhara.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichambua mche wa mti wakati wa
kuandaa vitalu kwenye mradi wa upandaji miti Kwesimu,Katibu Mkuu
alisisitiza watu kujali na kutunza mazingira yao .
0 maoni:
Post a Comment