ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA YAIBOMOA NGOME YA CHADEMA WILAYANI LUSHOTO



 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiutangazia umati wa watu waliofurika kwenye uwanja wa mikutano Sunga kurejea rasmi kwa Charles Kagonji (mwenye shati la kitenge) kwenye Chama Cha Mapinduzi akitokea Chadema,wengine katika picha hii ni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama
 Mzee Charles Kagonji akiwasalimia wananchi na kutamka rasmi kurejea CCM yeye pamoja na wafuasi wake aliokuwa nao Chadema.
Katika mkutano huu wengine waliorudi CCM kutoka Chadema ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo Ismail Semkunde,aliyekuwa Katibu wa Jimbo Mzee Julius Kavurai na aliyekuwa mgombea wa udiwani kwa tiketi ya Chadema Ndugu Ally Gaha
 Wananchi wakinyoosha mikono juu kama ishara ya kumkaribisha CCM Mzee Charles Kagonji
 Mzee Charles Kagonji akishukuru kurudi nyumbani CCM
 Mzee Julius Kavurai aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Mlalo Chadema akiwapungia mkono wananchi kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara wilayani Lushoto ya kujenga na kukiimarisha chama pamoja na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 inavyoendelea.
 Umati wa watu waliohudhuria mkutano.
 CCM juu!!!
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha juu kadi ya CCM tayari kumkabidhi Mzee Charles Kagonji ambaye ameorudi CCM kutokea Chadema.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya CCM Mzee Charles Kagonji kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Sunga jimbo la Mlalo wilayani Lushoto.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Mzee Charles Kagonji kwa uamuzi wake wa kurudi CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Ndugu Ismail Semkunde aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo la Mlalo Chadema na kuamua kurejea CCM.
  Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama akihutubia wakazi wa kata ya Sunga kwenye mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lushoto Balozi Abdi Hassan Mshangama (katikati) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Majid Hemed Mwanga (kulia) pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Jimbo la Mlalo Chadema Ndugu Ismail Semkunde.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment