Kesi imeanza dhidi ya mwanamume anayedaiwa kumuua na kumkataka vipande mpenzi wake mwanamume Jun Lin na kuwatumia wanasiasa vipande vya mwili wake kupitia kwa njia ya posta.
Inaarifiwa pia alitumia baadhi ya vipande vya mwili wa mwanamume huyo kwa shule kadhaa nchini humo.Luke Magnotta mwenye umri wa miaka 32 alifikshwa mahakamani mjini Montreal lakini alikanusha madai ya mauaji hayo yaliyotokea mwaka 2012.
Ikiwa atapatikana na hatia atafungwa maisha jela.
Mpenzi wa Magnota alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu raia wa China.
Polisi walianza uchunguzi wa mauaji hayo, baada ya kupata kiwiliwili cha mwanamume huyo karibu na nyumba ya Magnotta. Polisi walianza msako wa kimataifa kumtafuta Magnotta na hatimaye kumkamatia katika duka huduma za internet mjini Berlin Ujerumani.
Polisi walipata vipande vya mwili wa Lin katika posta vikiwa vimetumiwa waziri mkuu Stephen Harper pamoja na wasiasa wengine.
Polisi pia walipata vipande vingine vikiwa vimetumwa kwa shule mbili za kiingereza. Kicwa kilipatikana katika bustani la Montreal.
Kadhalika wachunguzi walipata video kwenye mtando ikionyesha mauaji ya Lin.
0 maoni:
Post a Comment