Jaji Mkabisa Tusi wa Afrika Kusini, amesema kua mashirika ya Consotium 4 Refugees and Migrants pamoja na shirika la Southern African Litigation
Center yameshindwa kuleta ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa nyaraka
za Kayumba Nyamwasa alizowasilisha kuomba hifadhi ya ukimbizi Afrika
Kusini zilikua na kasoro.
Pili Mahakama imesema mashitaka ya kumuhusisha Kayumba Nyamwasa na uhalifu wa kesi za kivita nchini Rwanda na DRC alipokua mkuu wa jeshi la Rwanda nayo hayana msingi .Jaji ameamrisha mashirika hayo mawili kumlipa Kayumba Nyamwasa gharama zote za kesi hii tangu ilipoanza kusikilizwa zaidi ya miaka miwili iliopita jambo ambalo waku wa mashirika hayo wamesema ni la kushangaza kuona Mahakama inayataka mashirika ya kutetea haki za kibinaadamu kulipa gharama za kesi hio.
Generali Kayumba Nyamwasa alishitakiwa na mashirika haya kuingia Afrika Kusini 2010 bila ya kupewa hifadhi ya ukimbizi.
Bwana Nyamwasa pia alishitakiwa kwa kuhusika na kesi za uhalifu wa kivita kwamba alikua afike mbele ya Mahakama ya kimataifa kujibu mashitaka hayo jambo ambalo mwenyewe amekua akisema yeye yuko tayari kujibu mashitaka hayo endapo serekali ya Afrika Kusini itakubali maombi hayo yasiokuwa na msingi.
0 maoni:
Post a Comment