Mwanaume
wa kwanza muingereza kuambukizwa homa kali ya Ebola, katika mlipuko wa
ugonjwa huo unaoshuhudiwa katika kanda ya Afrika Magharibi, anatarajiwa
kurejea Afrika ambako aliambukizwa.
Anasema anafanya hivyo ili aweze kuwasaidia wengine walioathirika kuweza kupambana na ugonjwa huo ambao ni janga kubwaWilliam Pooley alipokea matibabu mjini London baada ya kupelekwa nchini humo kutoka Sierra Leone.
Ameweza kupona na hata kuodnoka hospitalini. Lakini kwa sasa anajiandaa kusafiri kurejea Afrika katika wiki chache zijazo.
Wakati Pooley alipoambukizwa, alikuwa anafanya kazi ya kujitolea nchini Sierra Leone, ambayo ni moja ya nchi za kanda ya Afrika Magharibi zilizoathriwa na ugonjwa huo.
Takribna nusu ya watu 3,000 waliombaukizwa homa hiyo, katika mlipuko wa sasa barani Afrika, ambao ilianzia nchini Guinea, wamefariki.
''Nina hamu sana kurejea kufanya kazi inayonisubiri,'' Pooley aliambia BBC.
"nahisi kama zijaimaliza kazi yangu kwani niliondoka huko mapema sana. Na ninajua kuna kazi nyingi katika nchi hizo, na tunahitaji kuwa huko kuwasaidia watu. ''
0 maoni:
Post a Comment