Maafisa wa
utawala nchini India, wanachunguza ambavyo kitambulisho cha elektroniki
kimetengezwa kikiwa na picha ya Hanuman mungu wa kihindi na kutumwa kwa
njia ya posta.Kitambulisho hicho kina picha ya mtu anayejulikana
kama Hanuman kutoka kwa kipindi kilichojuolikana kama Ramayana, akiwa
amevalia mikufu ya dhahabu na taji la kifalme.
Kitambulisho
chenyewe kilipatikana wakati mfanyakazi wa posta alijaribu kukifikisha
kwa mtu aliyetumiwa ila hangeweza kupata anwani ya mtu yeyote
anayejulikana kama Hanuman.
Alipoangalia kwa picha , aligundua
kuwa huenda ilikuwa mchezo wa danganya toto. Bado haijaulikana ni nani
aliyeweka alama ya kidole kwenye kitambulisho hicho.
Hanuman
alijulikana kama mtoto wa mungu wa kihindi aliyejulikana kama Pawan, na
kitambulisho chenyewe kina namba ya simu na anwani ya sehemumoja katika
jimbo la Rajasthan.
Hanuman alijulikana kama mungu wa kihindi mwenye nguvu za ajabu na mtiifu sana
Kwa kawaida Hanuman huonekana akiwa na uso wa Nyani pamoja na mkia. Kuna hekaya za kale kuhusu Hanuman kote nchini India.
Mfanyakazi
huyo wa posta Heeralal Saini, alikirejesha kitambulisho hicho kwenye
kituo cha posta baada ya kukosa kumpata mtu kwa jina la Hanuman. 'Hanuman ni nani?'
Hanuman
ni mmoja wa miungu wanaobudiwa na watu nchini India na pia kuna hekaya
nyingi tu kwenye vitabu vya kihindi kumhusu. Huonekana kama binadamu
mwenye uso wa Nyani na mkia mrefu.
Mara kwa Mara yeye husemekana
kuwa mtoto wa mungu mwingine wa kihindi Pawan na anasifika kwa kuwa
mtiifu na mwaminifu pamoja na kuwa na nguvu za ajabu.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment