STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 16 Septemba, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Moroni, Comoro
Tanzania
imempongeza Rais wa Muungano wa Comoro Dk. Ikililou Dhoinine kwa
kuimarisha umoja na mshikamo miongoni mwa wananchi wa nchi hiyo ambapo
hivi sasa Comoro imekuwa na utulivu na amani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein amesema ni jambo la kujivunia kuona wananchi wa visiwa vya Comoro
wako katika utulivu, amani na wamekuwa bega kwa bega na Serikali yao
chini ya uongozi wa Rais Dhoinine.
Akizungumza
katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa kwa heshma yake na
mwenyeji wake Rais wa Muungano wa Comoro, Dk. Shein alisema ziara yake
nchini humo ina lengo la kuimarisha ushirikiano wa kihistoria na kindugu
uliopo baina ya wananchi wa Tanzania na Comoro.
Alimueleza
Rais Dhoinine na wageni waliohudhuria hafla hiyo kuwa amefurahishwa na
namna Serikali na wananchi wa Comoro wanavyothamini uhusiano wao na
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na ushirikiano na ndugu zao wa
Zanzibar.
“Najisikia
niko nyumbani kwa sababu uhusiano wetu umeimarishwa zaidi na mahusiano
ya wananchi wake kwa karne nyingi, mahusiano ambayo yamekuwa katika
masuala ya kijamii, utamaduni, biashara na mambo mengine mengi”
alibainisha Dk. Shein.
0 maoni:
Post a Comment