Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (wa nne kushoto) akipeana
mkono na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WENTWORTH inayochimba gesi
katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara , Robert MacBean (wa tatu
kushoto) mara baada ya kusaini Makubaliano ya Mkataba wa Kuuziana Gesi
kati yake na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC). Wengine
katika picha ni baadhi wa Watendaji Wakuu wa Wizara ya Nishati na
Madini, Shirika la maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC na wawakilishi wa
kampuni za WENTWORTH na MAUREL & PROM.
Wajumbe
waliohudhuria kikao cha Kusaini Mkataba wa Kuuziana Gesi kati ya
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Kampuni zinazochimba
gesi katika eneo la Mnazi Bay Mkoani Mtwara za WENTWORTH Resources
Limited na MAUREL & PROM wakisaini MKataba huo. Anayeshuhudia mbele
ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo pamoja na
wawakilishi wengine kutoka kampuni hizo, TPDC, Wizara ya Nishati na
Madini na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) James
Andilile (wa kwanza kulia) wakipitia Mkataba kwa pamoja na mmoja wa
wawakilishi wa Kampuni hizo wakati wa kusaini Mkataba huo. Katikati ni
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya MAUREL & PROM, Michael Hochard na wa
kwanza ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya WENTWORTH Robert MacBean.
0 maoni:
Post a Comment