Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nchi za nje
Philip Hammond,Uingereza haina njia nyengine
isipokuwa kujiunga na hujuma za madege ya nchi
shirika dhidi ya wanamgambo wa kigaidi wa dola la
kiislam-IS.Kwakua wanamgambo hao ni kitisho kwa
nchi yake na kwa utulivu wa eneo lote la Mashariki
ya kati,"watu hawana budi",anasema waziri huyo wa
mambo ya nchi za nje wa Uingereza.Bunge la
Uingereza linatarajiwa hii leo kupiga kura kama nchi
hiyo ishiriki katika hujuma za kijeshi za nchi shirika
nchini Irak.Inatarajiwa wengi wa wabunge wataunga
mkono mpango huo.Hammond ameondowa lakini
uwezekano kwa nchi yake kujiunga na hujuma hizo
dhidi ya wanamgambo wa itikadi kali wa dola la
kiislam -IS nchini Syria.Idadi ya raia wa Umoja wa
Ulaya wanaopigana upande wa magaidi wa kiislam
nchini Iraq na Syria inakisiwa imeongezeka na
kufikia watu 3000.Mapema mwaka huu idadi yao
ilikadiriwa kufikia waatu 2000.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment