- Walikuwa wanaenda kufanya usafi Polisi
- Walikwama hapo na kushindwa kuendelea kufanya usafi Hospitarili, Mahakamani Ofisi ya Mkoa
WAFUASI wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Njombe mkoani hapa wameshikiliw ana Jeshi la polisi kwa muda wa zaidi ya masaa matatu katika kituo cha Polisi kati kwa mahojiano.
Akizungimza na Na Mwandishi Wetu ElimtaaMkoani Njombe makamu mwenyekiti wa Chadema nyanda za juu Kusini, Alatanga Nyagawa alisema kuwa wafuasi hao walishikiliwa na jashe hilo wakati wakitaka kufanya usafi katika kituo cha polisi na makazi ya askali wakati wakianzimisha siku ya Nyerere Day.
Amesema kuwa watu walio kuwa wamezuiliwa na Polisi ni 9 akiwemo na diwani wa kata ya Njombe Mjini, Agrey Mtambo (Pichani) na viongozi wengine wa wilaya.
“Tulivyo taka kufanya usafi katika kituo cha polisi walitafsili kama ni kitu kibaya ambacho ni haramu hauwezi kusema kitu haramu wakati hakuna sheria inayoyema kitu hicho ni haramu, watapika kesi kwama tuliandamana polisi,” alisema Nyagawa.
Sauti ya Nyagawa hapa
- Na kuongeza kuwa “Wafuasi wetu walishikiliwa kwa muda wa masaa matatu hadi manne na walio shikiliwa ni Diwani, mwenyekiti wa wilaya, kamanda wa vijana Mkoa, na katibu wake na baadhi ya wanachama, na naona hii nia haikuwa njema sana,”
Nyagawa alisema wanachama hao walifika Polisi hapo kwa lengo la kufanya usafi katika maeneo hayo na huku wakianzia kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Njombe.
Maeneo waliyotarajia kufanya usafi ni Masoko ya Mjini, kituo cha mabasi na kituo cha polisi Stend, na kuwa ratiba yao ilikuwa wafanye usafi katika kituo cha Polisi kati na Mkoa, na kumalizia katika mahakama, na Hospitali teule Kibena ambapo walikwama Polisi wakiadhinisha Nyerere Day.
Hata hivyo walipo kuwa Polisi anasema kuwa hakuna maelezo yoyote waliyo chukuliwa na kuwa wametakiwa kurudi tena Octoba 20 baada ya kuachiwa kwa dhamana.
Aidha nyagawa alieleza sababu za kufanya usafi polisi ni kwasababu katika maeneo kama hayo yanamkusanyiko mkubwa wa watu na hata uzalishwaji wake wa taka ni mkubwa tofauti na maeneo ambayo hayana watu wengi.
Kwa kupande wake kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyani (Pichani) amesema kuwa atazungumza na waandishi wa habari leo kwa kuwa tukio hilo lilikuwa bado halija fika mezani kwake na kwa kuwa ilikuwa ni siku ya mapunziko hakuwepo ofisini.
0 maoni:
Post a Comment