KAMANDA wa polisi mkoa wa Njombe amesema kuwa siku ya kuazimisha kumbukumbu ya Nyerere, waliwashikulia na kuwahoji watu tisa wa Chadema wakiwa na diwani kwa kuingia katika kambi ya jeshi hilo bila kibali.
Akizungumza na Mwandishi wetu Elimtaa Kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe Fulgence Ngonyani alisema kuwa askali wake waliona watu walio kuwa wamevaasale za chadema wakiwa na gari aina ya pikup walitaka kufanya usafi katika kambi hiyo ambapo walikamatwa kwa kosa la kuingia bila kibali.
Sikiliza sauti ya Kamanda wa Polisi Njombe akitoa ufafanduzi wa wafuasi wa chadema walio shikiliwa, Kipande cha Kwanza (Bofya Play)
Amesema baada ya tukio hilo walipitia katika taarifa za jeshi hilo na kuona kuwa waliomba kibali cha maandamano na kukataliwa na kuomba kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya mji na kuruhusiwa na kuwa wakitane na uongozi wa maeneo husika.
Ngonyani ameongeza kuwa watu hao tisa jeshi hilo liliona wanakosa la jinai kwa kuvamia eneo la jeshi bila kutoa taarifa ya aina yoyote na kuwa wanaendelea na uchunguzi na kuwa watawafikisha mahakamani.
Sikiliza tena hapa>>>>>>>>>>(Bofya Play)
.jpg)
0 maoni:
Post a Comment