Idadi ya watu walioambukizwa na ugonjwa wa Ebola kaskazini
mwa Sierra Leone , upande
mwingine wa nchi hiyo ambako
maambukizi ya kwanza yalijitokeza miezi kadhaa iliyopita,
inaongezeka ambako kumekuwa na vifo vya watu 20 kila siku.
Maambukizi mapya ya Ebola yaliyothibitishwa hadi jana
Jumatatu katika kanda yenye ugonjwa wa Ebola nje na ndani
ya mji mkuu
Freetown imefikia 49. Kituo cha taifa cha
kupambana na ugonjwa wa Ebola kimeripoti leo, kuwa kuna
jumla ya watu 851 waliothibika kuwa na ugonjwa huo katika
kanda hizo mbili, ambazo ni eneo la magharibi ya mji na eneo
la magharibi la vijijini. Lakini hakuna maambukizi mapya katika
eneo la wilaya za mashariki za Kenema na Kailahun, ambazo
hapo kabla zilikuwa eneo lililozuka ugonjwa huo na ambapo kuna
watu zaidi ya 1,012 ambao wamethibika kuwa na ugonjwa huo.
Wakati huo huo chombo kimya kitawaruhusu madaktari
kumchunguza mgonjwa anayeshukiwa kuwa na virusi vya Ebola
katika muda wa dakika 15, na chombo hicho kinaweza
kupatikana katika nchi zilizoathirika na ugonjwa huo ifikapo
mwishoni mwa Oktoba.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment