Leo December 19, 2016 kutoka
Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Dar es salaam, mwanzilishi wa mtandao
wa kijamii wa JAMII FORUMS Maxence Melo ameachiwa kwa dhamana baada ya
kushikiliwa kwa zaidi ya siku 5 ambapo baada ya kupata dhamana hiyo Max
ameyaongea yafuatayo.
“Nawashukuru
mawakili wangu najua wamekuja kwasababu ya kutetea uhuru wa vyombo vya
habari, jukumu hili sio la Max peke yake ni jukumu la wote, Max amekuwa
mfano tu wakati mwingine atakuwa mtanzania yeyote anayetaka kutetea
uhuru wake, mimi sina shida na vyombo vya dola vinafanya kazi yake” – Maxence Melo
0 maoni:
Post a Comment