Leo December 19 2016 Waziri wa
sheria na katiba Dr. Harrison Mwakyembe alikwenda kwenye ofisi ya mkuu
wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda leo ambao kwa pamoja wametangaza
mipango mipya ya kuwasaidia Wananchi wa Dar es salaam kisheria.
Pamoja na mambo mengine waziri Mwakyembe
ameeleza jitihada mbalimbali ambazo wizara yake imekuwa ikizifanya
ikiwemo uanzishwaji wa mahakama ya makosa ya rushwa na uhujumu uchumi
ambayo ilianza kufanya kazi mwezi July na mpaka sasa ni kesi moja tu
ambayo imesikilizwa kwenye mahakama hiyo, Waziri Mwakyembe
amelizungumzia hilo….
‘Mahakama
imeshaanza kufanya kazi lakini baadhi wanahoji kuwa walitegemea kuwe na
kesi nyingi toka mwezi july ila tumekuja kubaini kwamba uchache wa kesi
ndio mafanikio makubwa ya hatua ya kisheria tuliyochukua, kwa sababu
sasa hivi wale waliozoea kupora pesa wamerudi nyuma ya kile kiwango
tulichokuwa tumekiweka’
0 maoni:
Post a Comment