Siku
chache kufikia siku ya utoaji tuzo za Soundcity MVP, Kituo cha TV cha
Sound City kimetangaza list ya kwanza ya wastaa wa muziki watakaoperform
kwenye sherehe hizo na zipo taarifa kuwa kutakua na suprise performance
ya mastaa kutoka Tanzania wametajwa kuperform siku hiyo.List
ya kwanza ya wasanii watakaopanda kwenye steji ya SoundCityMVP2016 ni
pamoja na Davido, Patoranking, Tekno, na Olamide huku mshereheshaji wa
siku usiku huo atakuwa ni Bright Okpocha a.k.a Basketmouth, comedian
kutoka Nigeria.
Kwa mujibu
wa waandaji wa tuzo hizo wameeleza kuwa list ya wasanii watakaoperform
siku hiyo itakuwa na mastaa kutoka Tanzania, South Africa na Nigeria
ambao wataonekana live kutoka kwenye ukumbi wa Expo Center, Eko Hotel
& Suites jijini Lagos, Nigeria.
Inaelezwa
kwamba zaidi ya watazamaji milioni 50 kutoka Afrika watashuhudia utoaji
wa tuzo hizo kwa njia ya TV pamoja na wale watakaokuwa live ukumbini.
Tuzo hizi zinatarajiwa kutolewa tarehe 29 December, na unaweza kuwapigia
kura wasanii kutoka Tanzania kwa kuingia hapa soundcitymvp.com.
Mwisho wa kupiga kura ni December 27, 2016.
0 maoni:
Post a Comment