Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeeleza lilivyojipanga katika kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa sikukuu ya mwaka mpya





Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeeleza lilivyojipanga katika kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa sikukuu ya mwaka mpya kuhakikisha wakazi wa mkoa huo wanaisherehekea kwa amani na utulivu 





DCP Dhahiri Kidavashari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamanda wa Polisi wa Mkoa Mbeya DCP Dhahiri Kidavashari amezungumza na wanahabari na kufafanua mkakati ambajeshi hilo limeuweka ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama katika nyumba za ibada, Kumbi za starehe, kwa waendesha bodaboda na vyombo vya usafiri pamoja na ulinzi na usalama katika makazi ya watu.

Amesema kwa makanisa ambayo yatakuwa na ibada za mkesha kwa siku ya tarehe 31.12.2016 kutakuwa na askari ambao wataimarisha ulinzi na usalama kwa kusaidiana na kamati ya ulinzi na usalama ya kanisa/msikiti husika. Kuhakikisha ulinzi ndani na nje ya kanisa/msikiti Kunakuwepo na ulinzi katika maeneo ya maegesho ya magari.

Amewataka wamiliki wa kumbi za starehe kufuata na kuzingatia taratibu za uendeshaji biashara zao hasa kwa kuzingatia muda wa kufungua na kufunga kumbi zao kulingana na vibali vya biashara zao, kuzingatia idadi ya watu wanaopaswa kuingia ukumbini kulingana na ukubwa wa ukumbi ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.

Pia Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewataka wazazi na walezi kuhakikisha kila mmoja anakuwa makini na mtoto wake kwa kutoa uangalizi katika kipindi chote cha sikukuu ya mwaka mpya.

Aidha Kamanda Kidavashari ametoa wito kwa wananchi kuacha kuzurura ovyo na pia kushirikiana na vikundi vya ulinzi shirikishi pamoja na kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu katika maeneo yao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment