Watu zaidi ya 50 wamefariki dunia na maelfu wengine kuachwa bila makazi baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha mafuriko yaliyopasua kingo za mto Kusini Magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.
DRC
Gavana wa Jimbo la Kati, Jacques Mbadu, amesema, mvua hizo zilisababisha mto Kalamu ambao unapita katika mji wa Boma kufurika maji kwa saa mbili ambapo baadhi ya miili imesombwa hadi mpakani na Angola.
Gavana Mbadu amesema, mpaka sasa wamezika miili 31 na kwamba wanatarajia kupata mingine 20 ambayo ilisombwa na maji upande wa mpaka na Angola baada ya mvua kunyesha kwa siku mbili mfululizo .
Amesema maji yalivuka kiwango chake na kufikia mita mbili na kuharibu nyumba takriban 500 katika mji huo wa Boma ambao uko jirani na mto Kongo kilomita 470 kusini magharibi mwa mji mkuu wa DRC, Kinshasa.