Maamuzi ya timu ya San Antonio Spurs kuhusu jezi ya Tim Duncan



Timu ya mpira wa kikapu Nchini Marekani, San Antonio Spurs inayoshiriki ligi ya NBA, imetangaza kuistaafisha jezi namba 21 aliyokuwa akivaa nyota wao wa zamani, Tim Duncan ambaye ametumikia timu hiyo tangu mwaka 1997 mpaka mwaka 2016 alipotangaza kustaafu.

Hii ilikuwa ni hafla ya heshima kwa Tim ambayo ilifanyika kwenye uwanja wa Spurs, AT & T Center, muda mchache baada ya timu hiyo kushinda kwa pointi 113-110 dhidi ya Pelicans kwenye uwanja huo.
Duncan ambaye anamiaka 40, akiwa na Spurs amefanikiwa kuchukua ubingwa wa NBA mara 5 (1999,2003,2005,2007,2014), na kushinda tuzo ya MVP wa ligi hiyo mara 2 (2002,2003).
.
Mmarekani huyo anakuwa ni mchezaji wa 8 wa Spurs jezi yake kustaafishwa, ameungana na kundi la George Gervin (44), David Robinson (50), Sean Elliott (32), James Silas (13), Avery Johnson (6), Bruce Bowen (12) and Johnny Moore
.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment