Benki Kuu ya Tanzania
imekanusha taarifa zinazozagaa katika mitandao mbalimbali ya kijami
kwamba noti za shilingi mia tano hazitatumika tena kuanzia Desemba 31,
2016 na kusema kuwa taarifa hizo siyo taarifa za kweli ni uvumi
unaopaswa kupuuzwa.
Noti ya shilingi mia tano.
Kwa
Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki (BOT),
Marcian Kobello amesema kuwa ukweli ni kwamba noti ya shilingi 500
itaendelea kuwepo katika mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500
hadi pale noti hiyo itakapotoweka mikononi mwa wananchi.
0 maoni:
Post a Comment