Wanafunzi Mabibo hatarini kuangukiwa na vigae



Jumla ya wanafunzi 600 wa shule ya msingi Mabibo iliyopo katika mtaa wa Mwongozo kata ya Makuburi jijini Dar es Salaam, wako katika hatari ya kuangukiwa na vigae
vilivyoezekwa katika shule hiyo ambavyo vimechakaa na kusababisha vigae hivyo kudondoka pia wanafunzi hao wamekuwa wakiloana nyakati za mvua wakiwa wanaendelea na masomo yao.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mwongozo Bwana James Ngoitanile ameiambia KURASA kuwa wamekwisha mwandikia barua Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ubungo kuhusiana na tatizo hilo ambalo linahitaji kushugulikiwa kwa hati ya dharura ili kubadilisha paa hizo ambazo zinahatarisha usalama wa wanafunzi.
Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bwana Hussein Milela amesema nyakati za mvua ofisi ya waalimu na vyumba vya madasara vinajaa maji hivyo kupelekea utoro kwa baadhi ya wanafunzi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment