WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA KUFANYA MTIHANI MWINGINE

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limesema kuwa wanafunzi ambao walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule za serikali nchini wanahitajika kufanya mtihani wa udahili tarehe 28 mwezi huu na wale watakaofaulu wataruhusiwa kujiunga na kidato hicho.
Taarifa hii ilitolewa kwa mara ya kwanza na Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde lakini kwa mujibu wa barua kutoka NECTA iliyosainiwa na Edgar Kasuga kwa niaba ya Katibu Mkuu kwenda kwa Makatibu Tawala wote wa Tanzania Bara siku ya Jumatatu, wale ambao hawatafaulu hawataruhusiwa kuendelea na masomo hayo ya sekondari.
NECTA inakusudia kutumia mtihani huo kuhakiki uwezo wa wanafunzi waliounesha katika kiwango chao cha ufaulu katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika mwaka jana. “Watakaofeli hawataruhusiwa kuendelea na masomo,” inasomeka sehemu ya barua hiyo. Makatibu Tawala wote, maafisa elimu na walimu wakuu wote wa shule za sekondari za serikali waliombwa kufikia leo wawe wamewasilisha orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na shule zao ili maandalizi yafanyike.
Afisa mmoja wa NECTA amesema maandalizi kwa ajili ya mtihani huo yanaendelea na kwamba wanafunzi wajiandae. “Maandalizi yanaendelea vizuri na tutatoa taarifa kwa umma kuhusu mabadiliko yoyote yatakayojitokeza,” alisema.
Katika Mtihani wa Taifa wa Kumaliza Elimu ya Msingi uliofanyika mwaka jana, watoto 789,479 waliofanya mtihani huo ambapo wanafunzi 555,291 walifaulu. Idadi hii ya waliofaulu ni sawa na asilimia 70 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani huo.
HT: THE CITIZEN

from Blogger http://ift.tt/2kceM4N
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment