Msanii wa muziki kutoka Dropout Entertainment, Linah Sanga ameamua kuweka wazi kuwa haoni tatizo kuacha tumbo lake lenye ujauzito wazi.
Linah amebainisha kuwa haoni tatizo na picha zake kwani ni za kawaiada sana, na pia hazina tatizo. Kauli hiyo ya Linah imekuja kufuatia comments za kejeli na matusi kutoka kwa mashabiki zake wakimtaka angefunika tumbo lake, na kuvaa dera kwani mimba ingeonekana tu.
”Siwezi kumfurahisha kila mmoja ndio maana anafanya kile ambacho anahisi kipo sahihi kwa upande wangu pia wkosoaji wapo wengi tu”amesema Linah ambaye wakati wowote anatarajiwa kuitwa mama.
Linah aliongeza kueleza kuwa, kwenye baadhi ya zile picha zipo ambazo alivaa kitenge, pia zipo alizojistiri kawaida.
0 maoni:
Post a Comment