Dar es Salaam. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kwa mfumo wa muungano uliopo, ni vyema kila upande ukawa unatoa rais kila baada ya miaka 10.
Amesema haiwezekani ziwepo nchi mbili zilizoungana halafu kila
akichaguliwa rais awe anatokea upande mmoja tu wa muungano, huku upande
mwingine ukiambulia kutoa makamu wa rais.
Mbali na hilo, Maalim Seif pia ametaja sifa tano za rais ajaye huku
akisisitiza kuwa kigezo si umri, bali uwezo wake wa kufanya kazi.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili Dar es Salaam,
Maalim Seif alisema:
“Kama ni muungano wa nchi mbili lazima kuwe na mfumo ambao tutajua
kwamba kipindi hiki rais ametokea Zanzibar, basi kipindi kingine rais
atatoka Bara.”
Tangu Tanganyika na Zanzibar zilipoungana na kuzaliwa Tanzania mwaka 1964, Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi ndiye pekee ambaye alitokea Zanzibar.
Aliongoza kati ya mwaka 1985-1995.
Akizungumzia Serikali ya Umoja wa Kitaifa kama inaweza kutumika Tanzania
Bara, kwa umakini Maalim Seif alisema, “Hilo ndilo suluhisho kutokana
na mivutano iliyopo Tanzania Bara. Serikali hii inaunganisha vipaji vya
watu ambao wanafanya kazi kwa pamoja.”
Sifa za rais
Huku akiwa makini na kuonyesha msisitizo wa ishara za mikono, Maalim
Seif alisema: “Kwanza rais awe na uwezo wa kuunganisha wananchi kwa
sababu ni wa Watanzania wote, kuanzia waliompigia kura na ambao
hawakumpigia kura.
0 maoni:
Post a Comment