KAMATI
Namba Tatu ya Bunge Maalumu la Katiba imependekeza mtu yeyote anayetaka
uraia wa kuandikishwa baada ya kufunga ndoa na Mtanzania, asipewe uraia
huo mpaka adumu katika ndoa husika kwa miaka 15. Akisoma
maoni ya wengi kutoka kwenye Kamati Namba Tatu bungeni jana, Dk Francis
Michael alisema kamati hiyo imependekeza kuwa Ibara ya 58
inayozungumzia uraia wa kuandikishwa ni vyema mmoja wa wanandoa awe na
sifa ya kuomba uraia baada ya kukaa kwenye ndoa kwa muda huo.
Dk
Michael alisema Ibara ya 58 inayozungumzia uraia wa kuandikishwa, ni
vyema mmoja wa wanandoa kuwa na sifa ya kuomba uraia baada ya kukaa
kwenye ndoa kwa muda huo.
Lengo la hatua hiyo ni kuondoa
udanganyifu wa watu kutumia mwanya wa ndoa, kupata uraia na kisha kupata
haki za kumiliki ardhi na rasilimali zingine.
Kamati Namba 10
pia ilitoa pendekezo katika ibara hiyo, ambapo Mwenyekiti wake Anna
Abdallah, alisema kamati hiyo imependekeza haki ya mwanandoa kupewa
uraia, itekelezwe baada ya kudumu katika ndoa miaka saba.
Rasimu
ya Pili ya Katiba, iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba
ilitambua wakazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wenye sifa za
kisheria kuomba uraia wa kuandikishwa, ikiwemo mtu aliyefunga ndoa awe
amedumu katika ndoa kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo.
Aidha,
kamati nyingi zimeonesha kuunga mkono pendekezo kumpa hadhi maalumu,
Mtanzania aliyekana uraia wake mara anaporejea nchini, ingawa zimepinga
kuwepo kwa uraia pacha.
Rasimu inampa hadhi maalumu mtu wenye
asili au nasaba ya Tanzania na ambaye ameacha kuwa raia wa Tanzania kwa
kupata uraia wa nchi nyingine, wanapokuja Tanzania kwa masharti
yatakayoainishwa na sheria za nchi.
Licha ya kutoa maelezo kuwa
kamati yake inatambua uraia pacha, Abdallah alisema wanapendekeza sheria
inayoainisha sifa na masharti ya mtu huyo anaporejea nchini.
Masharti
hayo ni suala zima la umiliki wa rasilimali, ambapo pia kamati hiyo
imependekeza watu hao kutoshiriki mchakato wa uchaguzi kwa kuchagua au
kuchaguliwa.
Akiwakilisha maoni ya wachache katika Kamati Namba
10, Said Arfi alisema wachache pia waliunga mkono kifungu hicho, ili
kuimarisha umoja, amani, uzalendo na usuala zimala usalama wa
nchi.HABARILEO
Home / Bongo
/ KUOMBA URAIA WA KUANDIKISHA KWA KIGEZO CHA NDOA KWA TANZANIA NI MPAKA ADUMU MIAKA 15.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment