BUNGE LA UTURUKI KUPIGA KURA KUIDHINISHA MCHANGO WAKE WA VIKOSI VYA MUUNGANO.

Kikao cha bunge la Uturuki kinajadili hii leo faraghani kuhusu pendekezo liliwasilishwa la kuidhinisha uingiaji wa wanajeshi wa serikali ya nchi hiyo katika vita dhidi ya wapiganaji wa kiislamu wa Islamic state nchini Iraq na Syria 

Wapiganaji wa kiislamu wameyateka maeneo kadhaa karibu na mpaka wa Uturuki na Syria na kutishia kuuteka mji wa Kikurdi wa Ain-al Arab mpakani na Uturuki.

Serikali ya kiislamu ya Ankara inasema ipo tayari kutoa mchango wake katika vita dhidi ya kundi la IS hata hivyo aijawekwa bayana kuhusu ushirika wake katika muungano wa kimataifa kulipiga vita kundi hilo la kijihadi.

Hayo yanajili wakati kundi la Islamic state likisanga mbele kwenye uwanja wa mapambano kuelekea kuuteka mji wa kobone licha ya mashambulizi ya vikosi vya muungano yanayoendelea.

Wapiganaji wa kikurdi wanaopambana katika mji huo muhimu kaskazini mwa Syria mpani na Uturuki wapo tayari kwa makubaliano ndani kwa ndani iwapo IS watafaulu kuuteka mji huo wa Ain-al Arab 

Kwa sasa wapiganaji hao wa kijihadi wapo kwenye umbali wa kilometa 2 pekee na mji huo Shirika la haki za binadamu linasema kunahofu ya kundi hilo kuuteka mji huo kwa muda wowote pia hofu ni uwezo wa wapiganaji wa kikurdi kulinda mji huo.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment