Mwanasoka wa zamani wa kimataifa wa Brazil Adriano Leite Ribiero ameshitakiwa kwa kuwa na uhusiano na wauza madawa ya kulevya mjini Rio de Janeiro.
Mwendesha mashtaka alisema mchezaji huyo alimpatia pikipiki muuza madawa ya kulevya ambaye ameitumia kwenye matukio ya uhalifu. Adriano mwenye miaka 32 yupo kwenye majadiliano na timu ya daraja la pili ya Le Havre ya Ufaransa. Tuhuma hizo ziliibuliwa mapema mwaka 2010 huku polisi nchini Brazil wakisema Adriano alinunua hiyo pikipiki mwaka 2008 na kuisajili kwa jina la mama wa muuza madawa huyo Paulo Rogerio de Souza Paz anayejulikana kwa jina maarufu la Mica. Pikipiki hiyo imekuwa ikitumika kusafirisha mihadarati katika vitongoji vya jiji la Rio na ikimilikiwa na genge maarufu la wahalifu la Commando Vermelho(Red Command).
Credit: BBC
0 maoni:
Post a Comment