Shirikisho la soka barani Afrika CAF lina wasiwasi kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Ebola,licha ya kukataa ombi la kuahirisha michuano hiyo ya mwaka 2015 barani Afrika.
Waandalizi wa dimba hilo nchini Morrocco wana hadi ijumamosi kuamua iwapo bado wanataka kuziandaa mechi hizo.
Wana hofu ya kuandaa michezo hiyo kutokana na mlipuko wa Ebola magharibi mwa Afrika.
''Tuna wasiwasi kuhusu hali yote'',alisema katibu mkuu wa Caf Hicham El Amrani.
''si hali nzuri kwetu sote''.
''Tunaelewa tahadhari ambayo taifa huru lina haki kuchukua,lakini ni muhimu kutoongeza hofu na badala yake kuwa wazi kuhusu vile unavyoweza kuambukizwa kutoka eneo moja hadi jingine huku tkichukua tahadhari'',.
''tumekuwa tukifanya kazi na shirika la afya duniani tangu mwezi aprili ili kuhakikisha kuwa hakuna hatari zozote.
Hatuwezi kujiweka katika hatari yoyote iwapo hatujui kwamba mashindano hayo ni tishio kwa mwandalizi''.aliongezea.
0 maoni:
Post a Comment