Kiasi cha pauni milioni 12
kimechangishwa nchini Uingereza ikiwa ni ombi kutoka kamati ya kupambana
na maafa kuwasaidia watu waliokumbwa na Ebola Afrika Magharibi,
michango hiyo ilichangwa kwa njia ya mitandao, simu na mchango wa
serikali ya Uingereza.
Kiasi hiki cha fedha kimechangwa baada ya
siku sita tangu ombi lilipotolewa na Idara hiyo,taarifa ya idara hiyo
imeeleza hii leo.Mkuu wa idara hiyo Saleh Saeed amesema wametiwa moyo mno na namna ambavyo Uma wa Uingereza ulivyojitolea kwa nia ya kuwezesha mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi na kuwashukuru kila mmoja aliyejitolea.
Idara za kupambana na maafa zinatoa mchango mkubwa Afrika Magharibi, ambapo mpaka sasa zimeshawasaidia watu milioni mbili na nusu walioathiriwa na Ebola ikiwemo kuwapa taarifa kupitia Kampeni za kutoa taarifa kuhusu ugonjwa huu.
idara za kupambana na maafa zimekua zikifika katika baadhi ya nchi zilizoathiriwa zaidi na Ebola na pia katika maeneo ya ndani yasiyofikiwa kwa urahisi ya nchini Sierra Leone na Liberia.
Mpaka sasa takriban watu 5,000 wamepoteza maisha na zaidi ya Watu 13,000 wanaugua ugonjwa huu, lakini wataalam wanasema takwimu hizi huenda zikawa kubwa zaidi kutokana kutotolewa taarifa za mara kwa mara.
Pauni milioni 12 zilizochangwa zinajumuisha Pauni milioni 5 zilizotolewa na Serikali ya Uingereza
0 maoni:
Post a Comment