UN:Hatuna raslimali za kudhibiti Ebola

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayesimamia kitengo cha kukabiliana na Ebola magharibi mwa Afrika ameiambia BBC kwamba hana raslimali za kuuthibiti ugonjwa huo.
Tony Banbury amesema kuwa msaada zaidi unahitajika kwa haraka ,licha ya mchango wa Uingereza,Uchina,Cuba na Marekani.
Lakini alikuwa na imani ya kuafikia malengo ya asilimia 70 ya vitanda kwa visa vipya na asilimia 70 ya mazishi kufikia mwezi Disemba.
Idadi ya vifo vilivyothibitishwa na shirika la afya duniani ni 4,818.
Idadi hiyo imeshuka tangu WHO kuripoti takwimu hizo awali ambapo shirika hilo linasema limebadilisha vile takwimu hizo zinavyochukuliwa.
Lakini imesema kwamba katika mataifa yalioathirika vibaya na mlipuko huo ikiwemo Liberia,Sierra Leone na Guinea,maambukizi yameendelea hususan katika miji mikuu
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment