JICHOPEMBUZI: Mkutano wa Umoja wa Afrika umefunguliwa Alhamisi Juni 11 nchini Afrika Kusini. Kaulimbiu ya mkutano huu wa 25 wa Umoja wa Afrika ni “ kuwawezesha wanawake ”. Mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi za Afrika wanashiriki mkutano huu utakaodumu siku mbili tangu Alhamisi wiki hii, kabla ya mkutano wa marais mwishoni mwa juma hili. Ushirikiano wa wanawake, lakini pia mgogoro nchini Burundi, migogoro mbalimbali inayolikabili bara la Afrika na masuala ya ugaidi ni miongoni mwa masuala nyeti ambayo yatazungumziwa katika mkutano wa 25 wa Umoja wa Afrika. Ni hotuba ya maamuzi chanya iliyotolewa na rais wa Tume ya Umoja wa Afrika Dlamini-Zuma katika ufunguzi wa mkutano huu. Dlamini-Zuma amekaribisha mkataba wa kuanzishwa kwa soko la pamoja kati ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, uliyoafikiwa nchini Misri wiki hii. " Hii ni hatua ya kwanza kuelekea kuundwa kwa eneo la biashara huria barani Afrika", ameongeza Dlamini-Zuma. Kuhusu suala la uhamiaji, " tunapaswa kukomesha safari hatari inayofanywa kila mwaka na maelfu ya Waafrika kuelekea Ulaya", amesema Dlamini-Zuma, huku akisihi " kuendeleza miradi mbalimbali barani Afrika kwa ajili ya ajira kwa vijana ". Dlamini-Zuma ametoa wito wa usafirishaji huru wa bidhaa na watu katika bara zima la Afrika. Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika ametoa wito kwa ajili ya ushirikiano zaidi wa wanawake, ikiwa ni kaulimbiu ya mkutano huu. " Kama tutaendelea kuunganisha wanawake katika kiwango cha sasa, itatuchukua miaka 80 kufikia usawa wa kijinsia katika nyanja mbalimbali. Tunapaswa kuwajibika zaidi ili kuhakikisha kuwa bara letu lina kuwa na maendeleo zaidi kwa kiwango cha kuridhisha. Na bara hili haliwezi kufikia hatua hii, kama hatuwashirikishi wanawake ", ameonya Dlamini-Zuma. Dlamini-Zuma hakuzungumzia kuhusu migogoro mbalimbali barani Afrika, ikiwa ni pamoja na hali inayoendelea Burundi, ambayo kwa hakika itatawala mazungumzo ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika. Suala la mgogoro nchini Burundi pia litajadiliwa Jumapili asubuhi na marais wa nchi kutoka bara la Afrika katika mkutano wa faragha kuhusu utawala. Wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa ugaidi Migogoro mingine inayolikabili bara la Afrika na ambayo itakua kwenye ajenda ya mmkutano huu ni pamoja na hali nchini inayoendelea Sudan Kusini, Libya, Nigeria na masuala ya ugaidi. Francisco Madeira, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Afrika dhidi ya ugaidi, amesema kutiwa hofu na kuongezeka kwa makundi ya kigaidi barani Afrika. TAGS: UMOJA WA AFRIKA AU - AFRIKA KUSINI - NKOSAZANA DLAMINI-ZUMA - BURUNDI - UGAIDI inShare Kuchapisha0 Tuma ukurasa huuKushirikisha JUU YA MADA HIYOHIYO AU-JOHANNESBURG-MKUTANO-USALAMA-SIASA Hali ya Burundi katika ajenda ya mazungumzo ya mkutano wa AU BURUNDI-AU-MAANDAMANO-USALAMA-SIASA Watu kadhaa wauawa katika vurugu Bujumbura BURUNDI-AU-DIPLOMASIA AU yakanusha kufukuzwa kwa mwakilishi wake Burundi SOMALIA-ETHIOPIA-MAPIGANO-USALAMA Somalia : watu 35 wauawa katika mapigano KENYA-AL SHABAB-MASHAMBULIZI-USALAMA Kenya : makabiliano kati ya polisi na wanamgambo wa Al Shabab NIGERIA-BOKO HARAM-JESHI-USALAMA Nigeria yachukua uongozi wa jeshi
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment