JICHOPEMBUZI: YANGA inaendelea kujifua katika mazoezi pale Karume yalipo makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mazoezi ambayo mashabiki wa timu hiyo wanaringia baadhi ya wachezaji wao wapya waliosajiliwa, lakini mmoja wa wapya hao usajili wake umeingia utata na huenda akaondolewa.
Yanga ilikuwa ikisaka kipa namba tatu atakayewapa changamoto wakongwe Ally Mustapha ‘Barthez’ na Deogratias Munishi ‘Dida’ na usajili huo ukamnasa kipa mmoja mrefu, Benedicto Tinocco, ambaye licha ya umbo lake kuwa tishio lakini uwezo wake unatia shaka kwa vigezo vya Yanga na huenda akaondolewa katika kikosi hicho. Taarifa kutoka ndani ya Kamati ya Usajili ya klabu hiyi zimesema Kocha mkuu, Hans Pluijm, hajavutiwa na uwezo wa kipa huyo aliyesajiliwa kutoka Kagera Sugar.
Bosi huyo alisema uwezekano wa Tinocco kuwapa changamoto Dida na Barthez ni mdogo. Kutokana na hatua hiyo sasa usajili katika nafasi hiyo ya kipa wakati wowote unaweza kufanyiwa masahihisho kwa kumtafuta kipa mwingine mwenye uwezo zaidi. Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha alisema:
“Tunaendelea kumfuatilia, lakini ni kweli kwamba makocha wetu hawajaridhishwa na uwezo wa Tinocco, ikishindikana tunaweza kuangalia hata kumtoa kwa mkopo.” Tizi lahamia ufukweni Wakati hayo yakiendelea Pluijm anaendelea na mazoezi ambapo kwa mujibu wa ratiba yake ya maandalizi, kesho Jumamosi kikosi hicho kitahamishiwa katika mazoezi ya ufukweni ili kusaka kusaka stamina kwa wachezaji kabla ya msimu kuanza. Barthez Barthez jana alimshusha pumzi za hasira Tiboroha baada ya kipa huyo kuanza mazoezi hatua ambayo inakuwa kama amempiga bao bosi wake huyo aliyepanga kumkata mshahara.
“Nilikuwa na matatizo kidogo ya kifamilia, lakini nashukuru uongozi umeelewa,” alisema Barthez. SC Villa kumpima Kamara Yanga itatumia mchezo wa kirafiki dhidi ya Villa ya Uganda wa Juni 27 kupima uwezo wa Lansana Kamara.
JICHOPEMBUZI - DESKTOP VIEWBACK TO TOP Soka Makala Za Burudani Kolamu Spoti Majuu
0 maoni:
Post a Comment