Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Singida, Martin Lissu akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Uchaguzi wa UVCCM Wilaya ya Singida Mjini juzi, Lissu alikemea vitendo vya rushwa ndani ya CCM.
Martin Lissu Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Singida.
Katibu wa UVCCM, Wilaya ya Singida Mjini, Pamfil James akisoma taarifa ya chama kwa wajumbe wa mkutano mkuu huo.
Wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Singida wakiwa wanasubiri matokeo ya uchaguzi huo.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa UVCCM Wilaya ya Singida Mjini.
Jafari Ikaku aliibuka kidedea, kwa kuchaguliwa kuongoza Jumuiya ya UVCCM Wilaya ya Singida Mjini.
Mmoja wa wagombea Seleman Moshi akimwaga sera kwenye uchaguzi huo.
Huyu mtoto ni tunda lijalo la CCM, alikuja kwenye uchaguzi huo akiongozana na baba yake mzazi Kessy ambaye ni mgombea Udiwani wa Kata ya Minga kwa tiketi ya CCM.(PICHA ZOTE NA HILLARY SHOO, SINGIDA).
Na Hillary Shoo, SINGIDA
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Singida amekemea rushwa katika chaguzi mbalimbali hapa nchini huku akisema kuwa anayetoa rushwa ili awe kiongozi, je endapo atachaguliwa kwa staili hiyo hizo fedha alizotoa atarejeshaje kama sio kuiibia serikali.
Mwenyekiti huyu Martin Lissu alitoa kauli hiyo mjini hapa wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Wilaya ya Singida Mjini kwenye ukumbi wa FDC Singida.
Aidha alisema kuwa katikia kipindeio hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu kumekuwepo na matukio mwengi sana ya rushwa miongoni mwa wagombea na kamwe katika uchuzi huo endepo itabainika mgombea kutoa rushwa attengua matokeo yake mara moja.
“ Mimi nachukia sana rushwa na niseme wazi kuwa nikibaini kuwa kuna mgombea ameshinda kwa kutoa rushwa kwa wajumbe, asilani asubuhi tu natengua matokeo yake, hatuwezi kuongozwa na watoa rushwa, na hili nalisema wazi , hata mimi nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wenu sikuwa hata na shilingi moja ndio kwanza nilikuwa natoka chuo kikuu.” Alisisitiza Lissu.
Lissu ambaye aligombea ubunge jimbo la Ikungi Mashariki na kushika nafasi ya pili, nyumba ya Jonathan Njau aliyeshinda, hata hivyo Kamati Kuu ya CCM ilitengua matokeo hayo na hivyo uchaguzi huo utarudiwa tenakutokana na kukiukwa kwa taratibu mbalimbali.
Aidha alisema CCM inaanzia katika ngazi ya familia kwani alama ya jembe na nyundo, hivyo itahakikisha watoto wa maskini watashinda katika chaguzi mbalimbali na ndio maana CCM imekuwa imara katika kudhibiti watoa rushwa kwenye chaguzi zake.
Akizungumzia Mwenyekiti wa CCM, Mgana Msindai kukihama chama na kujiunga na chadema huko ni kukosa dira na mwelelekeo, kwani nafasi ya uenyekiti aliyokuwa nayo Msindai ni kubwa sana ndani ya chama .
Lissu alisema Msindai amelijitia aibu, mkoa na Taifa kwa ujumla kwani ni mtu ambaye alikuwa akiheshimika sana ndani ya chama cha CCM lakini kwa kuwa ameona huko UKAWA kuna manufaa, anamtakia safari njema.
“UVCCM iko imara katika kuhakikisha inakilinda na kukitetea chama, hawa wazee wataendelea kubaki tu kuwa wazee wa Singida, vijana tupo na ninawahakikishia tutashika dola.” Alisema Lissu.
Katika Uchaguzi huo Jafari Ikaku alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Singida mjini baada ya kuwashinda wagombea wenzake nane.
from Blogger http://ift.tt/1J0tBxg
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment