Waandishi wa habari wahimizwa kuandika kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

WANAHABARI Nchini wametakiwa kuwa mabarozi wa uandishi wa
habari za mabadiliko ya tabia ya nchi ili kuiokoa dunia na mabadiliko ya tabia
ya nchi yanayo tokea kwa kasi.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya
hali ya hewa wa mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) Dr. Ladislaus Chang’a wakati
wa kutoa elimu kwa baadhi ya wakulima, wapima nvua na waandishi wa habari Mkoani
Njombe.
Alisema kuwa waandishi wa habari wanatakiwa kuhakikisha kila
mara wanawakumbusha wananchi kuhusiana na mabadiliko ya hali ya hewa na madhara
yake.
Alisema kuwa katika kipindi hiki waandishi wasipo wakumbusha
wananchi mara kwa mara juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi mazingira yataendelea
kuharibika, na joto kuongezeka maradufu.
Alisema kuwa baadhi ya wananchi hawajui juu ya mabadiliko ya
tabia ya nchi na kuwa mafuriko na kukosekana kwa mvua kunatokea kutokana na
kuwapo kwa upotevu wa misitu na ongezeko la moshi kutoka katika magari na
viwanda duniani.
Chang’a alisema kuwa waandishi waandike habari za uharibifu
wa mazingira, vyanzo vya maji na madhara yake ili wananchi kuelewa na kuendeleza
kupanda miti pasipo kukata miti.
Aidha nao waandishi walilalamikiwa kubandwa na wamiliki wa vyombo
vya habariu kwa kupewa mda mchache kwa mambo ya kutoa elimu kwa uma huku
wakitoa ushauri kwa mamlaka kubadilisha mfumo wa utoaji wa taarifa za utabili
wa hali ya hewa.
Raymond Francis alisema kuwa mamlaka inatakiwa kubadilisha
mfumo wa kutoa taarifa hizo kwa kuzirainisha ili kupata watu wanao zifuatilia
kwa wingi kuliko zinavyo tolewa na mda wa kutoa taarifa hizo.  
Francis alisema; “Mamlaka inavyo toa taarifa inatoa taarifa
ngumu watanzania wengi wanapenda vitu raini, nawashauri mgetumia watu wa
vichekesho watu wengi wangesikiliza, pia mda mlio weka wengi wanacheza na
rimoti za runinga zao kwa kuangalia vipindi vingine ingrpendeza kabla ya
taarifa ya habari au katikati ili watu kuziona taarifa hizo,” alisema.


from Blogger http://ift.tt/1JdeHqU
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment