Kwa hiyo, hatuna budi kutumia takwimu za nchi zilizoendelea kama Marekani na ulaji wa watu wake haupishani sana na baadhi ya Watanzania wanaoishi mijini. Baadhi ya tafiti za miaka ya 2008-2009 zinaonyesha kuwa nchini Marekani mtu mzima kwa wastani anakula sukari vijiko vya chai 22 kutoka katika vyakula vilivyosindikwa kiwandani.
Sukari ni chanzo muhimu cha nishati mwilini.
Bila sukari hakuna uhai. Kuacha kabisa kula vyakula vya wanga na vyenye sukari unaweza kusababisha mwili kuwa na kiwango kidogo sana cha sukari na kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo na viungo vingine.
Hali kama hiyo ikiendelea, mtu aweza kuishiwa nguvu na kupoteza fahamu na hata kifo. Hata hivyo, sukari nyingi ni sumu na inadhuru afya.
Ulaji wa sukari kupita kiasi unahusishwa na kuongezeka kwa unene, uzito kupita kiasi, ugonjwa wa kisukari cha ukubwani (aina ya pili), magonjwa ya moyo, baadhi ya saratani, kuoza kwa meno na ugonjwa wa ini.
Hatua ya kwanza ya kupunguza ulaji sukari ni kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu hatari ya kiafya inayotokana na ulaji wa sukari nyingi.
Matumizi ya sukari yanamfanya mtu awe anapenda sukari kama wale walio athiriwa na dawa za kulevya. Watu waache kutumia sukari hatua kwa hatua mpaka ulimi wao uzoee kutumia vyakula vyenye sukari kidogo au havina sukari kabisa.
Hatua ya pili ya kupunguza ulaji sukari ni kubainisha chanzo kikubwa cha sukari katika vyakula na vinywaji unavyotumia kila siku.
Baada ya kujua chanzo kikuu, weka mpango wa kupunguza ulaji wa vyakula hivyo. Kama unaweka vijiko vinne vya sukari katika chai au kahawa, punguza hatua kila wiki kijiko kimoja.
Baada ya wiki tatu utakuwa unakunywa chai na kuweka kijiko kimoja cha sukari.
from Blogger http://ift.tt/1N7PQI3
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment