USAFI WAFANYIKA MKUU WA WILAYA MKURUGENZI WASHIRIKI

Mkurugenzi ea halmashauri ya Njombe Paulo Malala akifanya usafi siku ya usafia katika hospitali lupembe.
Mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba, Akioanda maua siku ya usafi.
Baadhi ya eafanyakazi halmashauri ya wilaya ya Njombe wakifanya usafi 
……….the

ZOEZI la usafi wa mazingira lisiwe kikomo Disemba 9 na liwe endelevu na wananchi waone aibu kukumbushwa na rais masuala ya kufanya usafi na wananchi wametakiwa kukamata mtu anayetupa taka na kumtoza 50,000 na aliye mkamata kupata 25,000.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba wakati wa kilelecha siku ya uhuru ambayo kitaifa imeamuliwa na rais Dr John Magufuli kuwa siku ya usafi na kuwataka wakazi hao kuhakikisha zoezi la usafi linakuwa ni endelevu.

Alisema kuwa wananchi waone aibu kukumbushwa na Rais kufanya usafi wa mazingira kwani usafi wa mazingira ni kwaajili ya afya zao wenyewe na wasipende kuwa na maisha ya kuishi katika uchafu.

Dumba alisema kuwa anawapongeza wananchi wa wilaya hiyo kuto kutwa na maambukizi ya kipindupindu, kwa muda mrefu hiyi inatokana na kuwapo kwa usafi wa wakazi hao.

“Wananchi siku hii isiwe ni kilele cha usafi wa mazingira bali iwe ni siku kuhitimisha siku ya uhuru wa Tanganyika na usafi wa mazingira uweendelevu kila wakati” alisema Dumba.

Aidha alitoa msimamo wake kwa wilaya hiyo na kutoa amri ya watu kuwa walinzi wa wanao tupa taka huvyo na kukamatwa kama atamuona mtu anatupa taka hovyo na kutozwa shilingi 50,000 na aliye mkamata kupewa nusu ya pesa hiyo.

“Wananchi kama mtu atakamatwa kwa kutupa pea hovyo atozwa shilingo 50,000 uliye mkamata utapata shilingi 25,000 kutoka kwa afisa mtendaji wako na pea inayo baki inaenda katika mfuko wa halmashauri kwaajili ya utekelezaji wa shughuli za halmashauli” aliongeza Dumba.

Hata hivyo alisema kuwa endapo mtu atapatikana na kipindupindu atibiwe haraka na baada ya kupona apelekwe mahakamani kwa kura uchafu alipe faini ama afungwe kama hana pesa, na kuwataka madaktari wafanye kazi yao kwa ukamilifu kama wito wao ili mtu hiuyo apone.

Hata hivyo mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Njombe, Paulo Malala alisema kuwa wilaya hiyo ilikuwa ni ya pili kutaifa katika usafi wa mazingira kitaifa na kuwataka wananchi kutilia mkazo wa agizo la mkuu wa wilaya ya Njombe kuhakikisha kuwa wanamkamata mtu anaye tupa taka na kumtoza pesa hiyo na kuwataka watendaji kutoa pesa ya mtu aliye kamata mtupa taka papo hapo paada ya kupata malipo ya faini hiyo.

Naye mbunge wajimbo hilo aliwataka watumishi na wanazi wa jimbo hilo kuhakikisha kuwa wanakuwa na tabia za usafi huku akiwataka wakuu wa shule kuhakikisha kuwa katika kaeneo ya shule yanakuwa safi wakati wote vivyo hivyo katika maeneo ya hospitali.

Halmashauri ya wilaya ya Njombe imefanya usafi katika hospitali ya wilaya hiyo ya Lupembe na kupanda maua kuzunguka maeneo ya ofisi hiyo huku katika kila kijiji watendaji wake wakisimamia usafi wa mazingura.

from Blogger http://ift.tt/1QxzqJa
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment