Wahabeshi waliokamatwa hawa hapa..
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, akizungumza na waandishi wa habari.
JESHI la polisi mkoani Njombe linawashililia Wahabeshi 29 kutoka Ethiopia kwa tuhuma za kuingia nchini bila kibali pamoja na madereva wao 3 raia wa kitanzania maeneo ya Makambako mkoani humo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Wilbroad Mtafungwa alisema kuwa watu hao waliokamatwa ni wahabaeshi kutoka Ethiopia walikuwa wakeelekea mpaka wa Tanzania na Zambia ili waelekee nchini Afrika Kusini walikamatwa maeneo ya Makambako mkoani Njombe Juzi majira ya saa Usiku baada ya gari yao moja kuharibika ambapo walikuwana gari mbili.
Mtafungwa alisema kuwa askali wao walipata taarifa ya kuwa kuna magari mawili yaliyo kuwa yamebeba Waethiopia, ambao walikuwa wameingia nchini bila kuwa na kibali cha kuishi hapa nchini.
Alisema kuwa baada ya kufika katika gari hizo aina ya Toyota Haice zenye namba za usajili T 998 BGZ na ya pili Totota haice super Costume yenye namba za usajili T 371 DDR, na kuwa katika tukio hilo waliwakamata watu watatu walio kuwa wakisaidia na kuendesha magali hayo.
Alisema kuwa wahabeshi hao watafikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wao wakishirikiana na idara ya uhamiaji ili sheria kuchukua mkondo wake.
Hata hiyo madereva hao watatu wa kitanzania watakuwa na kesi ya kujibu kwa tuhuma za kuwasafilisha raia wa kigeni nchini na kuwasaidia kupita nchini bila kibali.
Aliwataja madereva hao walio kuwa wakisaidiana kuwa ni Issa Alli, Noeli Yohana wote wakazi wa Mikomi mkoani Morogoro na Juma Zuberi Mkazi wa Dar es Salaam.
Alisema kuwa baada ya uchunguzi kukamilika watawafikisha nao pia mahakamani na kuwa watanzania wawe makini kutokan ana watu wa aina hiyo kutokana na duniani kuwa na wimbi kubwa la Ugaidi hivyo taarifa za kuwapo kwa watu wa ina hiyo kutoa ili kuwa dhibiti kabla hawaja leta madhara.
Aidha mmoja wa madeva wa magari hayo Issa Ally alisema kuwa yeye hakuelewa kuwa alio wapakiza ni watu gani kutokana na yeye kuambiwa kuwa anawabeba watu wa harusi ambapo hakuweza kuwachunguza kutokana na kuwa ilikuwa ni usiku na mvua ilikuwa inanyesha.
Alisema kuwa walipo fika makambako Gari yao ilipata itirafu na kusababisha kusimama kwaajili ya matengenezo kabla ya kukamatwa na jeshi la polisi.
Hata hivyo Mmoja wa wahabeshi hao alisema kuwa wanaelekea nchini Malawi ambako wameambiwa kuwa kunakazi wametoka nchini kwa kutokana na ugumu wa upatikanaji wa ajira.
“Malawi kazi kidogokidogo ipo kazi tu kwetu hana kazi, hatuelewi Umetumia siku ngapi maka tuto hapa, hii ni mara ya kwanza kwenda Malawi, tunaambiwa kunakazi huko” alisema mhabeshi huyo.
from Blogger http://ift.tt/1NRcELF
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment