Kesi ya Uchaguzi Njombe inaendelea sasa inakaribia ukingoni

HATIMAYE ushahidi wa upande wa mshtakiwa katika kesi namba 6 ya uchaguzi mkuu ya mwaka 2015 nafasi ya ubunge jimbo la njombe mjini umefungwa katika mahakama kuu kanda ya iringa kwa shahidi mmoja kutolea ushahidi kati ya mashahidi wanne waliotajwa hapo awali.
Baada ya kukamilisha ushahidi huo katika kesi iliyofunguliwa na Emmanuel Masonga aliyekuwa mgombea ubunge kupitia Chadema dhidi ya Edward Mwalongo wa CCM ambaye alitangazwa kuwa mbunge wa jimbo la Njombe mjini, mahakama hiyo imeanza kusikiliza mashahidi watatu wa upande wa serikali ambao hata hivyo wanaendelea hapo kesho.
Aidha shahidi huyo wa mwisho kwa upande wa mshtakiwa Agnes Mbanga mkazi wa Idundilanga mjini Njombe alitolea ushahidi namna mkutano wa kampeni za ubunge wa chama cha mapinduzi zilivyokwenda hapo Oktoba 22 mwaka 2015 na kuwa Edwin Mwanzinga alieleza namna serikali ilivyofanyakazi ya kujenga barabara ya lami ya magereza, ukarabati wa zahanati ya Idundilanga  huku Edward Mwalongo akiahidi kuwasaidia kutatua tatizo la maji, kuwasaidia vijana kujikwamua na wimbi la umasikini pamoja na namna ambavyo anawasaidia watoto yatima.
Mara baada ya kukamilisha ushahidi huo wakili wa serikali aliwaita mashahidi watatu kwa upande wa serikali ambao ni Venance Msungu aliyekuwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi jimbo la Njombe mjini, Nelson Kyando ambaye alikuwa mjumbe katika kamati ya maadili wakati wa kampeni pamoja na William Myegeta ambaye alikuwa mmoja kati ya wagombea wanne wa ubunge katika jimbo la Njombe mjini Kutoa ushahidi wao.
Katika hatua nyingine mashahidi hao watatu walieleza namna ambavyo mchakato wa kampeni za uchaguzi mkuu ulivyokwenda na kwamba  ulikuwa wa huru na haki katika kipindi chote huku wengine wakikiri kuwa kulikuwa na mapingamizi ambayo hata hivyo tume iliyashughulikia vizuri.
Jaji wa mahakama hiyo Jacob Mwambegele aliahirisha kesi hiyo hadi kesho aprili 22 mwaka huu ambapo kesi hiyo inaendeshwa mfuruzizo bila kupitisha siku na  itakapoendelea kwa mashahidi wa upande wa serikali.
Nje ya mahakama Nipashe ilizungumza na wakili wa Edward Mwalongo  upande wa mstakiwa Samson Rutebuka kujua kwanini ameletwa shahidi mmoja pekee kati ya wanne walioelezwa hapo awali alisema huyo mmoja amewakilisha kila kitu ambacho kilitakiwa kujibiwa mahakamani hapo na kuwa hayo ni mambo ya kiufundi.
“Hiyo ndi mbinu ya kiufundi wa kisheria ambapo tumeona hoja zote zilizo takiwa kujibiwa na na mashahidi wangu zimejibiwa kwa kuwa ilikuwa ni lazima hoja zijibiwe lakini kwakuwa huyo mmoja amejibu kila kitu hakuna haja ya kusababisha wengine kujakuendelea kueleza kilekile,” alisema Rutembuka.

from Blogger http://ift.tt/1pk4eTE
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment