Madereva wagoma kutoa ushuru wa kutoka geti la stendi kuu ya Njombe


MADEREVA wa madasi yaendayo wilaya na mikoa jiranni ya Njombe
wamegoma kulipa ushuru wa geti la kutoka stendi hiyo kutokana na tope lililopo
katika eneo hilo la stendi na kuwapa shida abiria wao na kuiomba halmashauri
kufanya ukarabadi wa eneo la stendi kwa kujaza kifusi ili waendelee kulipa
ushuru.
Awali asubuhi jana madereva hao walipaki magari yao nje ya
stendi ikiwa ni njia ya kuishinikiza serikali kuondoa tope lililojaa katika
stendi hiyo na baadae kukubaliana kuingia stendi lakini kwa makubaliano ya kuto
lipa uhuru get nla kutokea.
Wakizungumza kwa jazba madereva, abiria na maafisa
usafilishaji wamesema kuwa haiwezekani halmashauuri hiyo kuendelea kuchukua
ushuru huku katika stendi hiyo hakuna marekebisho wanayo yafanya wakati
wanachukua ushuru.
Kelvini Nyepe ni moja ya viongozi wa wakatisha tiketi katika
stendi hiyo alisema kuwa waliamua kubadisha ambiria wao nje ya steni kutokana
na stendi hiyo kuwa na tope kama shamba la mpunga na kuwaonea huruma wateja wao
wanao safiri kuchafuka na tope hilo.
“Tulitoa mabasi yote nje ya Steni ili kuonyesha kuwa
hatukubali abiria wetu kuchafuka katika stendi hii lakini tumeona gari zikiwa
nje ya stendi hakuna usalama kwa kuwa kunaweza kusababishwa ajari kwa watu
wasio husikahivyo tumeamua kuingia stendi kwa sharti la kuto lipa ushuru hadi
stendi itakapo rekebishwa,” alisema Nyepe.
Mwenyekiti wa wasafiri shaji Laiton Mwaipopo aliesema kuwa kuwa
eneo hilo ni chafu na linahitaji marekebisho na kuwa wamefika katika ofisi za
halmashauri na kuahidiwa kuwa watarekebishiwa katika eneo hilo la stendi.
“tumeamua kuingiza gari ndani ya stendi kwaajili ya usalama
na tumekubaliana kuto lipa ushuru gali zote zitakazo  ingia ndani ya stendi hiyo,” alisema Mwaipopo.
Dereva wa Texi zinazo paki katika stendi hiyo alisema kuwa
wamekuwa wakikosa wateja tangu kuanza kwa tope hilo lililodumu kwa muda wa wiki
mili sasa na kuwa halmashauri haifanyi kufanya ukarabati kwa kuwa tepe
wanaliona lakini hawafanyii kazi na kuwa kila walipo wafuata wanaambiwa kuwa
stendi hiyo sio stendi na ipo eneo la Tanraod na wamewekeza nguvu kwenye stendi
mpya inayo jengwa.
Aidha mmoja wa abilia amesema kuwa eneo hilo limekuwa ni
chafu hadi kufikia hatua ya kubebwa mgongoni kutokan ana tope lililojaa huku
abiria wengine wakisubiri kupanda magari nje ya stendi ili kuto chafuka na
tope.
Kwa upande wa mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Mjini
Edwin Mwanzinga alisema kuwa ukarabati katika stendi hiyo utafanyika baada ya
kumalizika kwa mvua zinazoendelea kunyesha na kusema kuwa katika stendi hiyo
gari zinatembea ni afadhari kuliko barabara za vijijini hizo ndio zimejifunga
kabisa.
Hata hivyo mkurungenzi wa halmashauri ya mji wa njkombe
hakuweza kupokea siku ili kuzungumzia tatizo la stendi hiyo.

from Blogger http://ift.tt/1Sf4bpF
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment