Madereva Bajaji, Bodaboda 300 Makambako wafuzu mafunzo


JESHI la Polisi nchini limetakiwa kutoa elimu kwa madereva
pikipiki za magurudumu matatu na mawili maarufu kama  Bodaboda na Bajaji kuhusina na usalama wa
barabarani kabla ya kuanza kuwakamata kwa makosa hayo kitu kitakacho saidia
kupinguza ajali za Barabarani hapa nchini.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa Apec, Respicius
Timanywa wakati wa kufunga mafunzo kwa madereva bodaboda na Bajaji Halmashauri
ya mji Makambako mkoani Njombe, ambapo madereva 300 wamefuzu mafunzo ya usalama
barabarani na kuwatambua watekaji wa vyombo vyao.
Timanywa alisema kuwa haiwezekani madereva hao wakawa
wanakamatwa kabla hawaja patiwa elimu ya usalama barabarani kwa kuwa wanavunja
sheria hizo kwa kuto jua na kuwa baada ya kutolewa kwa mafunzo hayo jeshi la
polisi mkoani Njombe linaweza kuanza kufanya msako wa madereva ambao wamekuwa
hawata reseni na wasio fuata seria za usalama barabarani.
Alisema kuwa kwa elimu ambayo wamitoa madereva wahakikishe
kuwa wanazingatia wanapo kuwa barabarani na kujiadhali na zawadi vya kula
kutoka kwa wateja wao kwa kuwa Chungwa na pipi ni vitu vinavyo weza kuwekwa
madawa ya kulevya na kusababisha kutekwa na waharifu.
Aidha aliwataka madereva hao kutoa taarifa za waharifu kwa
jeshi la polisi pale wanapo ona kuna dalili za kuwapo kwa wahalifu kwa kuwa
vyombo vyao vimedaiwa kuhusishwa sana na uharifu hapa nchini.
Alisema kuwa kutokana na elimu wanayoitoa katoka mikoa 20
hapa nchini madereva walio wapatia elimu hakuna hata mmoja aliye pata ajali na
kuwa ajali za Pikipiki zimepungua.
Alisema kuwa mafunzo hayo yamesaidia kuwafanya madereva hao
kuwa na uhusioano mzuri na Jeshi la Polisi hapa nchini na kusaidia kufichua
wahalifu.
 
Akizungumzia upungufu wa ajali za barabarani zilizo kuwa
zikitokana na madereva Bodaboda Kamanda wa kikosi cha Usalama Barabarani Kelvin
Ndimbo alisema kuwa kwa sasa ajali zimepungua kabisa zinazotokana na madereva
bodaboda.
“Mkoa wa Njombe kutokana na elimu zinazotolewa na wadau
mbalimbali ajili za boda boda zimeisha kuna miezi ajali hizo hakuna kabisa hii
inaonyesha kuwa ajaili zilikuwa zinatokana kutokana na madereva wazembe,”
alisema Ndombo.
Mgeni rasimi katika Hafra hiyo ya kufunga mafunzo na
kukabidhi vyeti kwa madereva hao Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Njombe
Necodemus Katembo alisema kuwa kutokana na mafunzo waliyo pewa na shirika hilo
kuna uhakika wa kupungua kwa ajali na matukio ya uharifu kwa kuwa shirika hilo
mafunzo hayo yanatolewa ikiwa ni kwa mala ya pili.
“Naimani kwa sasa tumepata wakufunzi wengi nyinyi mkawe
waalimu kw

a wenzenu ambao hawajafika kwenye mafunzo haya, naamini kuwa mlikuwa
hamjui kuwa pikipiki zenu zinatakiwa kuwashwa taa hata mchana lakiji sasa
mnalitambua hilo kawaambieni na wenzenu,” alisema Katembo.

Baadhi ya madereva wamesema kuwa walikuwa wakisababisha
ajali kwa kuto jua baadhi ya sheria za barabarani na kuwa kwa sasa wanafahamu
alama zote za barabarani na kuomba mamlaka inayo husika na miundombinu ya
barabara kuhakikisha kuwa kunakuwepo na vibao vya alama za barabarani ili kuto
wasababishia ajali.

from Blogger http://ift.tt/1SJ4QxO
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment