Kocha
wa muda wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amesema
alirithi kikosi kibovu baada ya kutoka sare ya bila kufungana na
Slovenia katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia jana.
Southgate
alichukua mikoba ya Sam Allardyce mwezi uliopita kwa ajili ya kuisimamia
timu hiyo katika mechi zake nne ambapo mpaka sasa ameshinda mchezo
mmoja dhidi ya Malta kabla ya sare ya jana waliyopata. Uingereza ambao wanaongoza kundi F, walipata alama hiyo moja jana kufuatia juhudi za hali za juu zilizoonyeshwa na kipa wake Joe Hart.
Southgate amesema wakati alipoichukua timu haikuwa sawa lakini taratibu anaona kama kikosi hicho kinaimarika.
0 maoni:
Post a Comment