SONGWE
Baadhi ya wakuliama wa kijiji cha Idiwili
wilaya ya Mbozi mkoani Songwe wameiomba serikali iangaliea uwezekano wa
kupunguza bei ya mbolea ambayo kwa sasa ipo juu.
Wakulima hao wamemueleza mbunge wa jimbo la
Vwawa Jafeti Hasunga kuwa wanaomba kutekelezewa ahadi ya waziri wa
kilimo,mifugo na uvuvi Dk Charles Tizeba aliyoitoa mwezi septemba mwaka huu ya
kupunguzwa kwa bei ya mbolea.
Maandalizi ya kulima mashamba yameendelea
kushika kasi kwa wakulima katika kijiji cha Idiwili wilayani Mbozi wakulima
wanaandaa maeneo kwaajili ya kupanda mahindi.
Wakati wa makadilio ya bajeti ya wizara ya
kilimo na mifugo waziri mwenye dhamana Charles Tizeba amesema mfuko wa mbolea
ya kupandia utauzwa shilingi ishirini na nane elfu na mbolea za kupandia kilo
hamsini zitauzwa shilingi ishirini na sita elfu.
Baadhi ya maduka ya mawakala wa pembeje za
kilimo mjini Vwawa kutaka kujua kama wamepokea mbolea za bei nafuu.
0 maoni:
Post a Comment