Forodha ya Vietnam yakamata pembe za Ndovu kutoka Afrika

Forodha ya Vietnam yakamata pembe za Ndovu kutoka Afrika


Idara ya forodha nchini Vietnam imekamata kilo 619 za pembe za Ndovu kutoka Afrika zilizokuwa zimefichwa katika makontena mawili mjini Chi Minh nchini humo.

Habari zinasema, wafanyabiashara za magendo wamebuni njia mpya za biashara hizo, ambapo safari hii pembe za Ndovu zilifichwa katika shehena za mbao, ili kuepusha ukaguzi wa mionzi.

Mkutano unaojadili biashara haramu za wanyamapori ulifanyika hivi karibuni huko Hanoi nchini Vietnam, ambapo wajumbe walijadili namna ya kuimarisha hatua za kupambana na magendo ya wanyamapori na bidhaa zinazotokana na wanyama hao.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment