Watu 55 wauawa kwenye mapambano magharibi mwa Uganda

Watu 55 wauawa kwenye mapambano magharibi mwa Uganda


Watu 55 wakiwemo maofisa 14 wa polisi, waliuawa Jumamosi katika mapigano makali kati ya vikosi vya polisi na wapiganaji wanaomtii kiongozi wa jadi magharibi mwa Uganda.

Msemaji wa polisi nchini Uganda Andrew Felix Kaweesi amesema, washambuliaji 41 waliuawa katika mapigano hayo yaliyotokea kwenye eneo la Kasese.

Bw. Kaweesi amesema, wapiganaji wenye uhusiano na walinzi wa kiongozi wa kabila la Rwenzururu Charles Wesley Mumbere walishambulia vikosi vya usalama vilivyokuwa kwenye doria katika eneo la Kasese.

Wapiganaji hao wakiungwa mkono na wenzao wa kabila la Bakonzo kwenye sehemu ya mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo DRC, wanajaribu kuanzisha Jamhuri ya Yiira, ambayo itachukua ardhi ya Uganda na sehemu ya Kivu ya Kaskazini nchini DRC.

Jumapili vikosi vya usalama vilishambulia ikulu ya mfalme Mumbere na kumkamata. Hivi sasa kiongozi huyo amepelekwa Kampala ambako atakutana na rais Yoweri Museveni.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment