GARETH BALE HATAKUWEPO NA USITEGEMEE TENA KUMUONA MWAKA 2016


Kama ni shabiki wa klabu ya Real Madrid hususani mchezaji Gareth Bale ambaye ni moja kati ya wachezaji ghali zaidi duniani, taarifa hii ikufikie ambayo imetolewa leo kuhusu staa huyo wa kimataifa wa Wales anayeichezea Real Madrid ya Hispania.

Taarifa iliyotolewa leo kuwa Bale atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi minne, kufuatia upasuaji wa enka ya mguu wa kulia atakaofanyiwa kutokana na jeraha lake alilolipata katika mchezo wa UEFA dhidi ya Sporting CP uliomalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa goli 2-1.

Bale atafanyiwa upasuaji London na kuna uwezekano akaukosa mchezo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la dunia March 24 kati ya Wales dhidi ya Ireland utakaochezwa Dublin, Wales kwa sasa wapo nafasi ya 3 Kundi D linaloongozwa na Ireland akifuatiwa na Serbia kwa tofauti ya point 2.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment