Jamhuri yaweka pingamizi tena leo kwenye Rufaa ya Godbless Lema

Siasa

Jamhuri yaweka pingamizi tena leo kwenye Rufaa ya Godbless Lema


Rufaa ya mbunge wa Arusha mjini Godbles Lema iliyopangwa kutolewa leo imeshindikana baada upande wa Jamhuri kuweka pingamizi ya kuwasilisha notisi badala ya rufaa, ambapo Mbunge huyo amerudishwa rumande kwa ya mara tatu.

Upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiwakilishwa na mwanasheria Matenus J Marandu ambaye amesema wamefanya hivyo ili kuharakisha na wamekubaliana na pande zote mbili.

Wakili wa Chadema Peter Kibatala amesema wameshakamilisha taratibu za kisheria kuhusiana na pingamizi hilo na wanasubiri pingamizi hilo lililowekwa na upande wa serikali.

Jaji aliyekuwa akisikiliza pingamizi hilo Fatma Masengi ameelekeza upande wa serikali wawasilishe hoja zao kwa njia ya maandishi kabla ya November 30 ili aweze kutolea uamuzi December 2 mwaka huu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment