MAELFU WAAANDAMANA KUPINGA USHINDI WA TRUMP MAREKANI.

 








Maelfu ya watu wameandamana katika miji mbalimbali nchini Marekani kupinga ushindi wa Donald Trump wa chama cha Republican.
Wengi wamekusanyika nje ya jumba maarufu la rais huyo mteule Trump Tower mjini New York wakipaza sauti zao dhidi ya msimamo wa Bw Trump kuhusu sera za uhamiaji, mapenzi ya jinsia moja na haki ya uzazi yanayopingwa na Donald Trump.
Wanasema hata dunia ina wasiwasi juu ya ushindi wake.
Wameandamana licha ya Rais Obama kuhimiza umoja na Bi Clinton kuwaambia wafuasi wake kwamba Bw Trump anafaa kupewa "nafasi ya kuongoza".
Rais Obama anatarajiwa kukutana na Bw Trump baadaye leo katika ikulu ya White House ambapo watajadiliana kuhusu shughuli ya mpito na kupokezana madaraka.
Mamia ya waandamanaji wanaompinga Trump walikusanyika nje ya jumba kuu la Bw Trump, Trump Tower eneo la Manhattan jijini New York Jumatano jioni, wakibeba mabango yaliyokuwa na ujumbe "Not my president" (Si Rais wangu), pamoja na mabango mengine.
Polisi hapo awali waliweka vizuizi vya saruji pamoja na kuchukua hatua nyingine za kiusalama nje ya jumba hilo refu linalopatikana barabara ya 5th Avenue, jumba ambalo huenda likawa makao makuu ya Bw Trump wakati wa kipindi cha mpito kabla yake kuingia White House.
Image copyright Getty Images
Image caption Polisi wameweka vizuizi vya Trump Tower
Kuliripotiwa pia taarifa za waandamanaji kuziba lango la kuingia jumba la Trump Tower mjini Chicago Jumatano jioni, wakiimba: "No Trump, No KKK, No Fascists USA" (Hatumtaki Trump, Hatutaki KKK, Hatutaki Wafashi Marekani) na "Not my president!" (Si Rais wangu).
Mjini Oakland, California, na Portland, Oregon, waandamanaji waliteketeza bendera za Marekani.
Wakati wa hotuba yake baada ya kutangazwa mshindi mapema Jumatano, Bw Trump aliahidi kuponya vidonda vya migawanyiko, baada ya uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali, na kuahidi kwamba atakuwa "rais wa Wamarekani wote".
Msemaji wa White House Josh Earnest amesisitiza kwamba Bw Obama atakuwa na uwazi kuhusu kuhakikisha shughuli laini ya mpito atakapokutana na Bw Trump, ingawa aliongeza kwamba: "Sijasema kwamba utakuwa mkutano rahisi."
Image copyright Getty Images
Image caption Waandamanaji nje ya Trump Tower mjini Chicago
Rais huyo mteule atasindikizwa kwenda White House Alhamisi na mkewe, Melania, ambaye atakutana na Mke wa Obama, Michelle.
Image copyright Reuters
Image caption Mjini Los Angeles waandamanaji waliunda kinyago kinachofanana na Trump...
Image copyright Reuters
Image caption ... na baadaye wakakichoma.
Image copyright Reuters
Image caption Wanafunzi wa shule ya upili ya Berkeley wakiandamana kupinga ushindi wa Trump
Bw Obama, aliyempongeza mrithi huyo wake kwa njia ya simu mapema Jumatano, alisema si siri kwamba yeye na Bw Trump wana tofauti nyingi.
Lakini aliongeza kwamba wanataka kuhakikisha wanalinda maslahi ya taifa na kwamba alitiwa moyo na yale Bw Trump alikuwa amesema usiku uliotangulia.
Kundi la kushughulikia shughuli ya mpito la Bw Trump litaongozwa na Chris Christie, gavana wa New Jersey, na lina wiki 10 kukamilisha maandalizi hayo.
Image copyright Reuters
Image caption Wengi wameshangazwa na ushindi wa Trump
Rais huyo mteule, ambaye hajawahi kuhudumu katika wadhifa wowote wa kuchaguliwa au kuteuliwa serikalini, amesema kipaumbele chake kitakuwa kufufua na kuimarisha miundo mbinu ya nchi hiyo pamoja na kukuza ukuaji wa uchumi wa taifa hilo maradufu.
Mwenyekiti wa kitaifa wa chama cha Republican Reince Priebus alisema: "Donald Trump anachukulia hili kwa uzito sana," na kuongeza kwamba mfanya biashara huyo tajiri atatumia uwezo wake wa kutetea na kufanikisha mikataba ya kibiashara kuhakikisha mambo mema "yanatendeka kwa Wamarekani" haraka iwezekanavyo.
Image copyright Getty Images
Image caption Mwandamanaji mwenye bango nje ya jumba la Trump Tower, New York
Image copyright Getty Images
Image caption Waandamanaji California
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment