MKUTANO WA 4 WA KIMATAIFA WA AFRIKA NA NCHI ZA KIARABU WAFANYIKA NCHINI GUINEA YA IKWETA

Mkutano wa 4 wa kimataifa wa Afrika na nchi za Kiarabu wafanyika nchini Guinea ya Ikweta


Mkutano wa 4 wa Afrika na Nchi za Kiarabu umeanza jana katika mji mkuu wa Guinea ya Ikweta, Malabo, na kuhudhuriwa na viongozi 60 kutoka pande hizo mbili za mkutano.
Mkutano huo wenye kaulimbiu "Pamoja kwa maendeleo endelevu na ushirikiano wa kiuchumi", unalenga kutathmini maendeleo yaliyopatikana katika utekelezaji wa mpango kazi uliofikiwa katika mkutano wa 3 uliofanyika Kuwait mwaka 2013.
Akizungumza kwenye mkutano huo, rais Obiang Nguema Mbasogo wa Guinea ya Ikweta amesema kuna mambo mengi ya kufanana kati ya Afrika na nchi za kiarabu, kama vile historia, utamaduni na dini. Amesema anatarajia kuwa Afrika inaweza kujitokeza na kuongeza nafasi yake katika uwanja wa kimataifa.
Naye katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Ahmed Abou El Gheit amesema, hali ya usalama barani Afrika inahusiana na hali ya usalama kwenye nchi za Kiarabu, na anatumai kuwa pande hizo mbili zitaimarisha ushirikiano katika maeneo muhimu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment